Mashabiki wa Chelsea ya England wameonyesha hawana tofauti na wale wa Yanga na Simba hapa nyumbani baada ya kumvua jezi shabiki mmoja wa Manchester United.
Shabiki huyo aliyeelezwa kuwa raia wa Nigeria, alipotea njia na kwenda kukaa wa Chelsea wakati timu hiyo inaivaa Malaysia XI jijini Kuala Lumpur.
Mashabiki hao walionyesha kutofurahia shabiki huyo kuvaa jezi ya Man United iliyoandikwa Aon, wakaanza kuimba nyimbo za kumdhihaki na kutaka avue.
Mmoja rafiki zake ambaye alikuwa amevalia uzi wa Chelsea aliamua kukata mzizi wa fitna na kumvua.
Hali hiyo imekuwa ikijotokeza mara nyingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa mashabiki wanaopotea njia kama shabiki huyo wa Man United.
0 COMMENTS:
Post a Comment