Manchester
United imetua jijini Sydney nchini Australia kwa ajili ya ziara yake ikiwa
inajiandaa na msimu mpya.
Wachezaji kadhaa
wa timu hiyo wamekuwa kivutio kikubwa lakini Kocha mpya, David Moyes ameonyesha
ni tofauti na yule wa zamani, Alex Ferguson.
Tofauti kwa
kuwa alikuwa akifanya mambo kadhaa kama vile kupiga picha sehemu ambazo
zinamvutia.
Moyes
alipiga picha daraja maarufu la Sydney pamoja na jingo la Opera House ambalo ni
moja katika ya majengo maarufu duniani.
Kawaida Ferguson
amekuwa hatoi hata simu mfukoni wala kusumbuka kupiga picha, badala yake muda
mwingi amekuwa akifanya tofauti kabisa.
Lakini
Moyes ameonyesha si mtu wa kujivunga na anaweza kuwa huru kufanya mambo yake.












0 COMMENTS:
Post a Comment