July 14, 2013



Brian Majegwa akimtoka Ngassa.

Kocha Mkuu wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema hawezi kuingilia uhuru kiungo Brian Majwega kuzungumza na timu yoyote, lakini akamuonya.

Majegwa ,20, ambaye alitoa krosi safi iliyozaa bao lililoiua Taifa Stars katika mechi ya kuwania kucheza fainali za Chan Afrika Kusini, tayari Yanga na Simba zimeanza kumfukuzia.
Micho kazini.
Lakini Micho amesema Majegwa anayekipiga KCCA ya Uganda anaweza kuzungumza na timu yoyote lakini akamtaka kuwa makini na kuangalia jukumu lililo mbele yake la timu ya taifa.

“Hauwezi kumzuia mchezaji asizungumze na timu, mimi si kiongozi wa klabu yake. Lakini naweza kumuasa kama mwalimu wa timu ya taifa.

  “Kwamba mbele kuna jukumu zito ambalo lazima alitekeleze, la sivyo atakuwa katika sehemu ambayo si sahihi. Hivyo aangalia kuwa timu ya taifa sasa ina mechi muhimu ya marudiano.

“Asichanganye mambo lakini Yanga au Simba, kama wamevutiwa naye, wanaweza kuzungumza na klabu yake kwanza kwa maana ya kufuata utaratibu.

Tayari Yanga ndiyo zaidi imeonyesha kuvutiwa na kiungo huyo ambaye alikuwa kero kwa mabeki wa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic