| MAKOCHA WA ZAMANI WA YANGA, MICHO NA TIMBE WAKIWASILI LEO DAR NA KIKOSI CHA THE CRANES TAYARI KUIVAA TAIFA STARS... |
Kocha Mkuu
wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ametoa kali leo wakati akitua jijini Dar
es Salaam na kikosi chake cha The Cranes.
The Cranes
watakuwa wageni wa wanaume, Taifa Stars katika mechi ya kuwania kucheza fainali
za Chan itakayopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Micho
amesema hata kama Taifa Stars itakuwa nyumbani, bado kikosi chake ni bora zaidi
na wachezaji waliokuwa wanampa hofu ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu tu.
“Kweli
Taifa Stars ina kikosi kizuri, lakini hofu yetu kubwa ilikuwa Ulimwengu na
Samatta. Lakini sasa tutapambana vilivyo,” alisema Micho.
“Simaanishi
dharau kubwa, lakini ninaweza kusema tunataka kushinda hapa. Wala msitegemee
tutacheza kwa kujilinda.
“Mimi na
msaidizi wangu (Sam Timbe) si wageni na soka la Tanzania. Hivyo tutacheza na
tumejiandaa,” alisema.
Kikosi cha
The Cranes kimefikia katika Hoteli ya Sapphire iliyoko Kariakoo jijini Dar es
Salaam.
Mashabiki kadhaa
walijitokeza kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kuwapokea
wachezaji hao watakaovaana na Stars Jumamosi.







0 COMMENTS:
Post a Comment