Kiungo Mikel Obi
yuko njiani kujiunga na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba
anayekipiga katika klabu ya Galatasaray.Klabu hiyo ya Uturuki imekubali kutoa kutoa kitita cha pauni milioni 16 kumnasa Mnigeria huyo kutoka Chelsea,Obi ambaye ni kati ya viungo tegemeo wa Chelsea, alijiunga na timu hiyo mwaka 2006 na kusababisha sakata kubwa la usajili kati ya Manchester na Lyn Oslo ya Norway alikokuwa anatokea.
Kiungo huyo ameamua kuandoka katika kipindi ambacho kocha mpya Jose Mourinho ametua kuanza kuinoa timu hiyo ya London baada ya kurejea akitokea Real Madrid.







0 COMMENTS:
Post a Comment