September 5, 2016



Kikosi cha Simba kilichokwenda mkoani Dodoma kujiweka sawa kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara, kimerejea jijini Dar es Salaam jana Jumapili na kutamba kuwa ipo ‘full tank’ kwa ajili ya kutoa dozi katika mechi zilizo mbele yao.

Simba ilikwenda mkoani humo baada ya kupata mwaliko wa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hata hivyo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda, Jackson Mayanja, amesema kwamba kupata safari hiyo pamoja na kucheza mchezo huo wakati ligi kuu imesimama, imekuwa ni faida kubwa kwao katika kujiweka sawa na kurekebisha waliyoyaona katika mechi zao mbili za awali, hivyo sasa wamekuwa fiti zaidi katika kila sekta.

“Mazoezi na mechi tuliyocheza Dodoma imekuwa na mchango mkubwa kwa maandalizi na kujiweka fiti zaidi kwa ajili ya michezo inayokuja, imekuwa vyema kupata nafasi ya kuja sehemu kama hii wakati ligi imesimama na kupata muda wa kurekebisha tuliyoyaona kwenye mechi za awali za ligi.

“Bado safari ni ndefu na ligi ina mechi nyingi, kwa hiyo unapopata nafasi kama hii na unapoitumia vizuri, inaleta faida kubwa kwa mechi za baadaye, ukizingatia msimu huu tunahitaji kufanya vizuri zaidi,” alisema Mayanja.


Mpaka sasa, Simba imecheza mechi mbili za ligi, ya kwanza waliumana na Ndanda na kushinda kwa mabao 3-0, mechi ya pili wakatoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu, jumla imekusanya pointi nne. Keshokutwa Jumatano wanatarajia kucheza dhidi ya Ruvu Shooting.

1 COMMENTS:

  1. hizo ndiyo mechi zenu za mchangani na matopeni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic