NIZAR (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI YANGA NA NADIR HAROUB... |
Kiungo nyota wa Yanga, Nizar Khalfan
amepata msiba baada ya kufiwa na baba yake mzazi.
Marehemu pia ni baba wa kiungo wa Coastal
Union, Razack Khalfan ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga.
Khalfan Khalfan amefariki dunia leo
jioni katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Nizar amethibitisha msiba huyo wa baba
yake mzazi na kusema huenda mazishi yatakuwa Jumatatu.
“Sasa tunaendelea na kujadili kuhusiana
na mipango ya mazishi lakini kwa taarifa za awali mazishi yanaweza kuwa
Jumatatu saa 10 jioni,” alisema Nizar ambaye pia aliwahi kucheza soka la
kulipwa katika nchi za Kuwait, Canada na Marekani.
0 COMMENTS:
Post a Comment