July 12, 2013



BALOTELLI ENZI ZAKE AKIWA NA RAFAELLA ALIYEWAFIKISHA WAZAZI WAKE KIZIMBANI...


Mzazi mwenza wa mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli, amewafikisha wazazi wa mshambuliaji huyo mahakamani kwa kumkashifu.

Raffaella Fico, 25, amewafikisha mahakamani wazazi hao wa Balotelli, 22, kwa madai ya kumdhalilisha wakiamini ni mtu anayejali fedha kuliko utu.
 
...AKIWA NA MPENZI WAKE WA SASA FANNY NAGUESHA ALIYEMVISHA PETE YA UCHUMBA

Mwanamitindo huyo na Balotelli wamezaa binti anayeitwa Pia lakini hivi karibuni mwanadada huyo alizungumza na waandishi na kusema mshambuliaji huyo wa zamani wa Man City amekuwa hawajali hata kidogo.

Kitendo hicho kimeonyesha kumuudhi Rafaella na sasa anawapandisha kizimbani Franco na Silvia Balotelli.

Rafaella aliyewahi kuwa mpenzi wa Criatiano Ronaldo kabla ya kuhamia kwa Balotelli, aliachana na mtukutu huyo wakati wa majira ya joto, siku chache kabla ya kuzaliwa kwa Pia.


Sasa Balotelli ana kitu kipya, mwanadada aitwaye Fanny Naguesha, raia wa Ubeligiji mwenye asili ya Nigeria.

Balotelli tayari amemvalisha Naguesha pete ya uchumba ambayo imeelezwa ina thamani ya pauni 100,000 (zaidi ya Sh milioni 240).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic