![]() |
| TAMBWE AKIMWAGA WINO MBELE YA HANS POPE |
Mshambuliaji nyota wa Vital’O, Hamis Tambwe amesaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.
Tambwe amesaini mkataba huo leo mbele ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.
Tambwe aliwasili nchini juzi kwa ajili ya mazungumzo
na Simba na alisema yeye si mchezaji wa majaribio badala yake atafanya
mazungumzo na Simba.
Tambwe aliibuka mfungaji bora wa michuano ya Kombe la
Kagame lililofanyika nchini Sudan hivi karibuni baada ya kufunga mabao sita.
Pamoja na hivyo Tambwe aliisaidia Vital’O kubeba
ubingwa kwa kuifunga APR ya Rwanda kwa mabao 2-0, yeye akifunga moja katika
fainali.
Tambwe pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa michuano
hiyo ambayo timu za Tanzania na Kenya zilijitoa kwa kuhofia usalama.









0 COMMENTS:
Post a Comment