*Kaburu,
Hans Pope wahusika, wakata mawasiliano
Vita ya kumnasa kiungo nyota mshambuliaji wa Uganda,
Moses Oloya inazidi kushika kasi na sasa Simba imeamua kufanya fitna kwa
kumtumia mshambuliaji wake wa zamani, Emmanuel Okwi amalize mchezo.
Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kumwania Oloya
anayekipiga katika kikosi cha Klabu ya Saigon Xuan Thanh ya
Vietnam, lakini Yanga nao ‘wakatia mguu’.
Kwa kuwa Yanga waliamua kuingia na kuanza kazi ya
kumnasa Oloya likiwa ni ombi la kocha wao, Ernie Brandts, aliyesisitiza
anamhitaji Mganda huyo, Simba wameamua kumtumia Okwi ambaye pia amemsisitiza
Oloya kuwa sehemu sahihi ni Simba.
Chanzo cha uhakika kimeeleza, Simba ilimtuma Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ kwenda Uganda ambako alifanya mazungumzo na Oloya kwa mara
nyingine akiwa katika kambi ya The Cranes.
“Kaburu ambaye alikwenda kwa niaba ya (Zacharia) Hans
Pope ambaye mwanzo ndiye alizungumza na Oloya. Pia alimtumia Okwi amshawishi
Oloya kuhusiana na Simba na maisha yake yalivyo, najua atakuwa amemueleza Yanga
hakumfai.
“Kweli Okwi alifanya naye mazungumzo na kumsisitiza
kama anataka kuja Tanzania, basi timu sahihi ni Simba. Kwangu sidhani kama
kweli Oloya anaweza kubadilika maana ni rafiki wa karibu wa Okwi,” kilieleza
chanzo hicho cha uhakika.
“Okwi na Oloya wanaelewana sana, wamekuwa marafiki kwa
kipindi kirefu. Hivyo dalili zote zinaonyesha kuwa Oloya atatua Simba.”
Yanga ilifanya juhudi hadi kumtuma mwakilishi nchini
Vietnam kuhakikisha inamnasa, lakini viongozi wake walikanusha baada ya kuona
mpango umejulikana na Oloya aliwataka watoe dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni
160) kama alivyokuwa amewaeleza Simba.
Kuona hivyo, Simba wakaongeza nguvu kwa hofu ya
kumkosa. Timu hizo zinalazimika kusubiri mkataba wake umalizike ili atue nchini
na kila upande bado unamhitaji. Taarifa zinadai nyota huyo atatua nchini Agosti
28, mwaka huu.
SOURCE: CHAMPIONI








0 COMMENTS:
Post a Comment