| KIGGI (KULIA) AKIWA NA SIMBA |
Klabu ya Simba imeamua kukata mzizi wa
fitna na kumpeleka kiungo wake Kiggi Makasi kutibiwa nchini India.
Taarifa za Kiggi kupelekwa India
zimepatikana jioni hii jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wa
Simba, Evodius Mtawala.
Mtawala amesema suala hilo si geni
lakini tayari uhakika kuwa Kiggi atakwenda India kwa matibabu.
“Tayari tuliishatangaza kuhusiana na
kumpeleka India na tulichokuwa tunasubiri tupate nafasi kwa daktari bingwa.
“Sasa ndiyo ametueleza na maandalizi
yameanza, hivyo Agosti katika terehe iliyopangwa atakwenda India kwa ajili ya
matibabu,” alisema.
Kutokana na kuona Simba wamechelewa
kumpeleka India, Kiggi aliamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mjini Bagamoyo.
Kiggi aliamua kuutibu mguu wake huo
alioumia wakati Simba ikiwa mkoani Dodoma katika mechi ya kirafiki dhidi ya
CDA.







0 COMMENTS:
Post a Comment