![]() |
| Wenger akiwa na Stojkovic... |
![]() |
| Stojkovic wakati akiwa mchezaji wa Grampus... |
Mfaransa huyo alikuwa kocha wa timu ya Nagoya Grampus, safari hii amerudi na timu yake hiyo ya England ambayo ilimuona akiwa mjini hapa na kumpa kazi.
![]() |
| Wenger akipokelewa... |
Wenger ametua mjini hapo na kupokelewa kwa heshima kubwa huku akiaminika ndiye kocha kutoka Ulaya kwenye mafanikio makubwa zaidi kuliko wengine waliowahi kuifundisha Nagoya.
Wenger ambaye alipokelewa kwa heshima kubwa alisifia hatua kubwa waliyopiga kisoka.
Lakini kivutio kikubwa zaidi
kilikuwa ni kocha wa Nagoya Grampus, Dragan
Stojkovic ambaye alisajiliwa na Wenger katika nafasi ya ushambuliaji wakati
yeye akiwa kocha.
Walipokutana katika meza wakati
wanazungumza na waandishi wa habari, Wengwer alionyesha kuwa ni mwenye furaha
kumkuta mwanafunzi wake akiwa ndiye kocha wa timu yake hiyo ya zamani.
Hali hiyo inaonyesha ujuzi wa kocha huyo
umeendelea kuwa kumbukumbu kwa mashabiki ambao wanamchukulia kama shujaa.














0 COMMENTS:
Post a Comment