July 2, 2013



 Kiungo nyota wa Corinthians, Paulinho amemwaga chozi hazarani baada ya kutangazwa kwamba amejiunga na Tottenham.

Paulinho aliyekuwa mmoja wa nyota walioisaidia Brazil kutwaa Kombe la Mara kwa kuifunga Hispania kwa mabao 3-0 amejiunga na Spurs kwa uhamisho wa pauni milini 17.1.




Katika mechi ya fainali dhidi ya Hispania ambao ni mabingwa wa Dunia, Paulinho aliwapa wakati mgumu viungo nyota kama Xavi na Iniesta na kufanikiwa kuvuruga kabisa mfumo wao.



Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alitangaza kujiunga kwake huko na Spurs ambayo imetumia zaidi ya mwezi kupambana ili imnase ili akapige kazi katika mitaa ya London.

Kocha wake, Andre Villa Boas maarufu kama AVB alisisitiza kumnasa kiungo huyo ambaye alikuwa gumzo katika michuano ya Kombe la Mabara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic