Mshambuliaji wa Man United, Robin van Persie ameonyesha si mkali wa kupachika mabao pekee, badala
yake hata katika mpira wa meza maarufu kama table tennis au ping pong.
Van Persie alifanikiwa kuonyesha ujuzi
baada ya kumshinda beki kisiki wa United, Rio Ferdinand.
Wawili hao walicheza mchezo huo wakati
wakiwa kambini nchini Australia ambako Manchester United iko katika ziara ya
kujiandaa na msimu mpya.
Katika mchezo huo, van Persie aliibuka
na ushindi wa pointi 11-9 dhidi ya Rio ambaye alianza kwa kasi lakini akapozwa
taratibu.








0 COMMENTS:
Post a Comment