July 18, 2013


Uongozi wa klabu ya Azam FC umeonyesha kusikitishwa na kauli alizozitoa kiungo Abdulhalim Humud wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM.

Azam FC imeamua kumlipa Humud kila alichokuwa anadai na kumpa nafasi ya kuwa huru na kuendelea na mambo yake.

Humud alilalaumu kutoelewa mambo kadhaa kuhusiana na mustakabari wake, huku akieleza kama Azam FC walionyesha kutoweka mambo kadhaa wazi kuhusiana na uhamisho wake.

Lakini kupitia mtandao wake, Azam FC imeonyesha kuwa ilikamilisha kila kitu kuhusu Humud na alishasaini mkataba na Jomo Cosmos iliyo daraja la kwanza nchini Afrika Kusini.

Ufafanuzi wa Azam FC ulikuwa hivi;

1. Ana Barua Mkononi aliyopewa na Uongozi wa Azam Kumfahamisha kuwa yupo huru kujiunga na Jomo Cosmos.

2. Ana mkataba mkononi aliosaini kati yake na Jomo Cosmos,

3. Azam FC wameshamwaga wino kwenye transfer contract kumruhusu akajiunge na Jomo Cosmos on free transfer tangia April 2013.

4. Analalamika eti Azam FC inatangaza kumuondoa kwenye usajili kwa kuwa ameuzwa South Afrika badala ya kufurahi.

5. Analalamika eti Azam FChaijamsafilisha… tangia lini uliona timu inayomuuza mchezaji inamsafirisha? Kimsingi wa kuulizwa ni Jomo Cosmos kwa nini hawatumi ticket.

6. Muda wa usajili bado unaendelea tena unafungwa Septemba yeye analalamika kwenye vyombo vya habari badala ya kwenda klabuni kuuliza hatma yake.

7. Ili kumpa uhuru wa 100% Azam FC leo imeamua kumlipa kilichobaki kwenye mkataba wake na kuachana naye ili kumpa uhuru kamili… sasa ni mchezaji huru… wanaosema Azam FC inambania sijui wanatoa wapi hizo hoja? Mbaya zaidi hata wale waliomhoji hawajathubutu kutafuta ukweli upande wa pili… hii yote inaonesha kuwa waliomhoji walikuwa na lao jambo au hawajui misingi ya objective jounalism ambapo kama mwandishi ni lazima uweke habari yako kwenye mizania kwa kuhoji pande zote mbili.

8. Tunamtakia kila la kheri Abdulhalim Humoud katika maisha yake kama mchezaji huru 100%.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic