Azam Media Group imeingia Mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Simba
Sports wenye thamani ya Sh milioni 331.
Mkataba huo utaiwezesha Azam TV kurusha kipindi katika runinga yake kitakachokuwa
kinajulikana kama Simba TV.
Mkataba huo umesainiwa leo na pande zote mbili, Simba ikiwakilishwa na Mwenyekiti
wake, Ismail Aden Rage na Katibu Mkuu, Evodius Mtawala pamoja na Mjumbe wa
Baraza la Wadhamini, Hamisi Kilomoni.
Wakati upande wa Azam Media Group uliwakilisha na Abubakar Bakhresa ambaye ni mkurugenzi mkuu, Meneja
Mkuu, Said Mohamed na Mwanasheria wake, Shani Christoms.
Katika hafla
hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kibo ndani ya jengo la PSPF
jijini Dar es Salaam, Simba walikabidhiwa hundi hiyo ambayo ilipokelewa na Rage.
Kabla ya hapo, Azam TV pia ndiyo imekuwa na nafasi kubwa ya kupata nafasi
ya kuonyesha live Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Azam TV ambayo itaanza kurusha matangazo yake hivi karibuni, imetenga
dola milioni moja, zaidi ya Sh bilioni 1.6 ili kupata tenda hiyo ambayo ilikuwa
inachuana kwa kasi SuperSport ya Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment