July 3, 2013




Beki wa Yanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Yondani amezawadiwa kitita cha Sh milioni tano katika hafla ya kukabidhi washindi iliyofanyika katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Azam FC,  Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast pia amelamba Sh milioni 5 za Vodacom kutokana na kupachika mabao mengi zaidi ya mwingine.
 

Kocha Abdallah Kibadeni amepewa tuzo ya kocha bora na kubeba Sh milioni 7.5. Mkongwe huyo kazoa tuzo hiyo baada wakati akiwa kocha wa Kagera Sugar msimu uliopita na sasa anainoa Simba.

Kipa, David Burhani wa Prisons ya Mbeya, ametangazwa kuwa kipa bora na kuzima ndoto za Ally Mustapha ‘Barthez’ wa Yanga ambaye aliaminika angetwaa tuzo hiyo.



Mabingwa Yanga wamezawaziwa Sh milioni 15 kutokana na kuwa timu yenye nidhamu bora zaidi katika ligi hiyo huku zawadi ya mchezaji mwenye nidhamu ikienda kwa Fuli Maganga wa Mgambo Shooting ya Tanga alipewa Sh milioni 5 pia.

Picha za tukio zima kuhusiana na tuzo hizo za Ligi Kuu ya Vodacom, tutawaletea baadaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic