YANGA imefanikiwa kuibuka na ushindi
wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi ya kirafiki iliyofanyika leo
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo mabao ya Yanga yalipatikana kupitia kwa Said Bahanuzi katika dakika ya 24, Jerry Tegete dakika ya 80 na Hussein Javu katika dakika ya 87, wakati lile la Mtibwa lilifungwa na Shaban Kisiga dakika ya 57.
Katika mchezo huo, uliohudhuriwa na
mashabiki wengi kiasi, kikosi cha Yanga kilikuwa hivi:
1
Deogratius
Munishi 'Dida' 2.Juma Abdul 3.Oscar Joshua 4.Nadir Haroub 'Cannavaro' 5.Issa
Ngao 6.Athuman Idd 'Chuji' 7.Said Bahanuzi 8.Salum Telela 9.Jerson Tegete
10.Shaban Kondo na 11.Haruna Niyonzima .
Walioanzia benchi ni 1.Ally Mustapha
'Barthez' 2.Yusuph Abdul 3.Ibrahim Job 4.David Luhende 5.Rajab Zahir 6.Bakari
Masoud 7.Hussein Javu 8.Abdallah Muhi 9.Nizar Khalfani na 10.Hamis Kiiza.
WACHEZAJI Said Bahanuzi, Hussein Javu na Jerry Tegete
leo wameizamisha Mtibwa katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment