Real Madrid imeichapa Everton ya
England mabao 2-1 katika mechi iliyopitwa mjini Los Angeles, Marekani na
kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la International Champions.
Mshambuliaji wake nyota, Cristiano
Ronaldo ndiye aliongoza mashambulizi ikiwa ni pamoja kufunga bao la kwanza
wakati Mjerumani, Mesut Ozil akipachika la pili na la ushindi.
Kutokana na ushindi huo, Madrid
inayofundishwa na Carlo Ancelotti inasubiri mshindi kati ya wakali wawili AC
Milan au Chelsea ambazo zitacheza nusu fainali nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment