Kiungo
nyota wa Tottenham, Gareth Bale ameishuhudia timu yake ya taifa ya Wales
ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland akiwa kwenye benchi.
Kocha
Mkuu wa Wales, Chris Coleman amethibitisha kuwa kweli Bale ni majeruhi ndiyo
maana aliamua kumkalisha katika benchi akiwa na suti yake kama mtazamaji.
Mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali dhidi ya majirani hao ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Lakini
wachambuzi wanaona suala hilo kama kuna ujanja na huenda Bale anafanya hivyo
ili kuendeleza kampeni zake za kutaka kujiunga na Real Madrid.
Inaonekana
kuwa Bale asingeweza kucheza mechi hiyo kwa kuwa tayari alishaileza Spurs
kwamba yeye ni mgonjwa.
Hivyo
amekuwa akikwepa kujiunga na Spurs ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuendeleza
kupewa ruhusa ili ajiunge na Madrid.











0 COMMENTS:
Post a Comment