Mshambuliaji
mpya wa Simba, Betram Mombeki yuko katika hatari ya kuongezeka uzito na kupungua
kasi nchini kutokana na kula vyakula ambavyo si sahihi kwa wanamichezo.
Mombeki
ambaye ameonekana kuwa tegemeo katika upachikaji mabao kwa washambuliaji wa
Simba, alionekana katika mgahawa mmoja katika eneo la Mlimani City akila
chakula ambacho ni kuku wenye mafuta kwa wingi maarufu kama ‘junk food’.
Akiwa katika
mgahawa huo, Mombeki aliyeongozana na kiungo Humud Abdulhalim ambaye hakuka
chakula.
Baada ya
Mombeki kuchukua chakula hicho na
kuongozana na Humud katika maegesho ya magari ambako walipanda gari aina ya
Mazda rangi ya bluu lililokuwa likiendeshwa na Humud.
Kwa mujibu
wa madaktari na mitandao maalum ya afya, vyakula hasa kuku wa mafuta wanaouzwa
katika migahawa maalum ni hatari sana.
Wachezaji
wanaocheza ligi kubwa barani Ulaya wamekuwa wakikatwa na madaktari.
Junk food
au kwa jina jingine la fast food huongeza haraka sana mafuta (fat) mwilini
ambayo huzunguka vifaa maalum vya mwili kama moyo.
Moyo wenye
mafuta ni hatari kwa mwanamichezo yoyote kwa kuwa unakuwa umebanwa wakati
unatakiwa kuwa huru.
Lakini kuongezeka
uzito si kitu kizuri kwa mchezaji, kwani pamoja na kusababisha kasi yake
ipungue, lakini uzito mkubwa unaweza kuchangia kuumia kwa viungo kama magoti na
kifundo cha mguu ‘enka’.








0 COMMENTS:
Post a Comment