Mshambuliaji
mpya wa Yanga, Mrisho Ngassa ambaye anakabiliwa na sakata la uhamisho kutoka
Simba, amenunua gari jipya aina ya Toyota Prado.
Gari
hilo linalokadiriwa kufikia thamani ya Sh milioni 50, ameanza kulitumia
takribani wiki sasa na amekuwa akienda nalo mazoezini.
Prado
la Ngassa ni ghali zaidi kuliko magari yote yanayotumiwa na wachezaji na
makocha wa timu hiyo.
Kocha
Mkuu, Ernie Brandts pia anatumia Prado lakini thamani yake ni chini kidogo
ukilinganisha na lile la Ngassa kwa kuwa yanapishana model na mwaka wa
kutengenezwa.
Kabla
Ngassa alikuwa akimiliki gari aina ya Nissan ambalo alianza kulitumia baada ya
kuliuliza lile la Toyota Verrosa alilokuwa amepewa na Simba baada ya kujiunga
nayo.
Simba
inaeleza ilimpa gari hilo na fedha ili kuongeza mkataba wa mwaka mmoja baada ya
kuwa limemchukua kwa mkopo kutoka Azam FC.










0 COMMENTS:
Post a Comment