Bango linalomuonyesha kiungo Gareth Bale
wa Tottenham kwa ajili ya kutangaza Ligi Kuu England katika jiji la New York
limeondolewa haraka.
Bango lililokuwa nje ya ukumbi maarufu
wa Times Square limeondolewa ikiwa ni siku moja tu baada ya Bale kuchelewa
mazoezini.
Kuchelewa kwake mazoezini kumeelezwa ni
sehemu ya vituko anavyofanya akiwa amepania kwenda Real Madrid.
Inaonekana sasa umefikia wakati Bale
hatazuiliwa kwenda Madrid na hata televisheni ya NBC iliyokuwa imeweka bango
hilo imelitoa ikiamini Bale sasa atakuwa mshiriki wa La Liga na si Premiership.








0 COMMENTS:
Post a Comment