Aidha, pamoja na
Coastal kucheza mechi hiyo ya kirafiki na Bandari, pia itacheza mechi nyingine
mbili na timu za nchini humo kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara
inayotarajiwa kuanza Agosti 24, mwaka huu.
Mashambulizi ya kikosi cha Coastal msimu huu yataongozwa na kiungo Haruna Moshi 'Boban' ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Simba.
Hemed Morocco
ambaye ni Kocha Mkuu wa Coastal, aliliambia Championi Jumatano kuwa, wameamua
kuchagua kucheza na timu za Kenya akiamini timu za huko zina ushindani mkubwa,
hivyo zitawajenga kisoka.
“Tutacheza mechi
tatu za kirafiki tukiwa Mombasa, tayari tumeshafanikisha mipango ya kucheza na
Bandari lakini pia tutacheza na nyingine mbili kwa ajili ya kujiweka vizuri
zaidi.
“Unajua timu za
kule ni nzuri kwa ajili ya ushindani wao mkali mara zote unapokutana nazo, kwa
hiyo itatusaidia sana sisi kujijenga na baadhi ya vitu kwenye soka,” alisema
Morocco.
Coastal pia
itatumia ziara hiyo kwa ajili ya kuweka kambi nchini humo ambapo bado
haijawekwa wazi itakuwa ni ya siku ngapi.







0 COMMENTS:
Post a Comment