Mchezaji wa
zamani wa timu ya Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Godfrey Bonny
‘Ndanje’, ametua timu ya Lipuli FC ya
Iringa na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo.
Bonny amemaliza
mkataba wa kuitumikia timu ya Saoswat Youth Club ya nchini Nepal msimu
uliopita, hivyo amerudi nchini na kumwaga wino Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja
la Kwanza.
Akizungumza na Championi
Jumatano, katibu mkuu wa klabu hiyo inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Yanga,
Shadrack Nsajigwa, Willy Chikweo, alithibitisha uwepo wa mchezaji huyo klabuni
hapo.
“Kila kitu
kimeshakamilika, tayari tumeshamalizana na Bonny na amesaini mkataba wa mwaka
mmoja kwa ajili ya kuitumikia klabu yetu katika msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza,”
alisema Chikweo.
Lipuli kwa sasa
ipo katika mikakati mizito ya kuirejesha timu hiyo Ligi Kuu Tanzania Bara tangu
iliposhiriki mara ya mwisho kwenye ligi hiyo msimu wa 1998/99.








0 COMMENTS:
Post a Comment