Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa),
limemtangaza mshambuliaji we Bayern Munich, Frank Ribery kuwa mchezaji bora wa
Ulaya kwa msimu uliopita.
Ribery raia wa Ufaransa amechukua tuzo
hiyo na kufanikiwa kuwashinda nyota Lionel Messi wa Barcelona na Cristian
Ronaldo wa Real Madrid.
Ribery amepata kura 36 zilizomuwezesha kushika nafasi ya kwanza, Messi ameshika nafasi ya pili akiwa na kura 14 na Ronaldo akashika namba tatu akiwa na kura 3.
Messi pekee alikuwepo katika tuzo hizo wakati Ronaldo kama ilivyo kawaida yake hakuonekana.
Messi pekee alikuwepo katika tuzo hizo wakati Ronaldo kama ilivyo kawaida yake hakuonekana.
Mara kadhaa, Ronaldo amekuwa
akishindwa kutokea hasa katika tuzo anazojua hawezi kubeba.
0 COMMENTS:
Post a Comment