Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro, amewaambia wachezaji wapya
waliosajiliwa na timu hiyo kuwa, mchezaji mvivu hatapata nafasi kwenye kikosi
chake.
Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo ni Mrisho
Ngassa, Hussein Javu, Rajab Zahir, Deogratius Munishi 'Dida', Shaabani Kondo na
Hamis Thabit.
Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha huyo alisema ili mchezaji
apate nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, ni lazima ajitume mazoezini.
Minziro alisema, pia nidhamu ya mchezaji inahitajika nje na ndani
ya uwanja ili kutimiza vizuri majukumu atakayopewa kwenye mechi.
“Wachezaji wapya tuliowasajili wanatakiwa watambue kuwa ili wapate
nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, wanatakiwa wasiwe wavivu wa
mazoezi.
“Ili mchezaji apate nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lazima
ajitume ndani ya uwanja, pia nidhamu inahitajika ndani na nje ya uwanja,”
alisema Minziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment