Staa wa Barcelona, Lionel Messi alilazimika
kuweka majukumu yake ya uwanjani pembeni kwa muda nchini Thailand na kujumuika
na watoto wenye ulemavu kwa ajili ya kucheza na kufurahi nao pamoja.
Messi ambaye ni mshindi mara nne wa
tuzo ya Ballon d'Or alijumuika na watoto hao ambao wengi wao walionekana
kufurahia uwepo wake kwenye kituo chao hicho ambapo, Messi alikuwa pamoja na
kipa wa Barcelona, Jose Manuel Pinto ikiwa ni sehemu ya majukumu ya Unicef ambao
ndiyo walioandaa utaratibu wa shughuli hiyo.
Wachezaji hao walisaini vitabu na
jezi za kumbukumbu za watoto hao kwenye kituo hicho kilichopo jijini Bangkok
Barcelona ipo nchini humo ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya msimu ambapo itakipiga dhidi ya timu ya taifa ya Thailand,
kesho Jumatano huku Neymar aliyesajiliwa kwa pauni milioni 50 kutoka Santos,
hivi karibuni akiwa ni mmoja ya mastaa watakaocheza mechi hiyo.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment