![]() |
| AKIAGWA NA OFISA WA FIFA... |
Na Saleh Ally, aliyekuwa Zurich USWISS
Mtanzania Damas Ndumbaro ametua katika makao makuu ya Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa), tena kimyakimya.
Championi lililokuwa na mwaliko katika makao makuu ya shirikisho
hilo jijini humo, baadaye lilimuona Ndumbaro akiingia kwenye mkutano na baadhi
ya maofisa wa shirikisho hilo.
Dakika kadhaa, alitoka na kuingia katika chumba kingine ofisini
hapo ambako alikaa kwa takribani dakika 15 na kutoka.
Alipoulizwa kilichompeleka Fifa, Ndumbaro ambaye ni wakala wa
wachezaji anayetambuliwa na shirikisho hilo, alisisitiza kwamba mambo yote
yanabaki kuwa siri yake na maofisa hao.
Kuhusiana na tetesi kwamba ana mpango wa kugombea nafasi ya urais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoshikiliwa na Leodegar Tenga kwa sasa,
Ndumbaro alisema:
“Huu ulikuwa ni mwaliko maalum, kuna mambo mengi ya muhimu
kuhusiana na maendeleo ya soka la Tanzania. Sidhani kama ni sahihi kwenda
kwenye vyombo vya habari kwa kuwa yanahitaji utekelezaji kwanza.
“Mimi nakushauri usubiri, acha niingie katika utekelezaji halafu
baadaye nitazungumza ni nini hasa,” alisema.
Ofisa wa Fifa aliyekuwa anamuaga Ndumbaro na kumkabidhi vitabu vya
Fifa, pia aligoma kuliongelea suala hilo na kusisitiza anayeweza kufanya hivyo
ni Ndumbaro.
“Mwenyewe anaweza kulizungumzia hilo, mimi kazi yangu ilikuwa ni
kumkaribisha na kumuaga,” alisema huku akimkabidhi vitabu na makabrasha kadhaa
yaliyoandikwa Fifa.
Ndumbaro aliwahi kugombea nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF
lakini akashindwa kwa kura chache na Ramadhani Nassib na sasa inaelezwa huenda
akagombea nafasi hiyo ya Tenga ambayo tayari Jamal Malinzi na Athuman Nyamlani
wamejitokeza.









0 COMMENTS:
Post a Comment