Kocha mpya Barcelona, Gerardo Martino amekiri kwamba kikosi chake bado hakijawa katika hali anayoiihitaji.
“Kweli tumecheza na kushinda katika mechi za majaribio, lakini kiwango haikuwa kizuri.
“Hata mashabiki waliokuja katika mechi zetu watakubaliana nasi kwamba hatukuwa katika fomu nzuri.
“Lakini tutajipanga, mambo yatakuwa tifauti tutakapoanza msimu na mechi yetu na Levante hakika tutafanya vizuri sana,” alisema kocha huyo maarufu Tata.
Tata amechukua nafasi ya Tito Vilanova ambaye ameshindwa kuendelea na kazi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa.








0 COMMENTS:
Post a Comment