Beki wa zamani wa Simba, Said Ndikumana
‘Koko’ amesema Simba imelamba dume kwa kumsajili Kaze Gilbert ‘Demunga’ raia wa
Burundi.
Kokoo raia wa Burundi pia aliyeichezea
Simba miaka mine iliyopita, amesema Demunga ni kati ya mabeki bora wachache wa
kati katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Awali nilisikia Simba wanataka
kumsajili, nikajua wanaweza wakachukulia kawaida tu.
“Lakini wamekuwa siriaz, kweli wamepata
beki mzuri sana, ni mchezaji wa uhakika na ana uwezo mkubwa.
“Uchezaji wa Demunga ni kama Victor
Costa, anapenda kutuliza mpira, anajiamini na ni mzuri kwa mipira ya vichwa. Kama
watakaa naye vizuri, ninaamini watafurahia sana,” alisema Kokoo.
Kwa sasa Kokoo yuko mapumzikoni
nyumbani kwao Bujumbura na anatarajia kurejea Oman alikokuwa anacheza soka la
kulipwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment