Beki David Luiz amezua tafrani katika
klabu yake baada ya kumueleza Jose Mourinho kwamba anataka kuondoka na kujiunga
na Barcelona.
Luiz raia wa Brazil amezua mkanganyiko
huo na kusisitiza anataka kuondoka ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya
kuanza kwa Ligi Kuu England.
Awali Barcelona ilitangaza kulipa pauni
milioni 25, Chelsea ikaona ni kama kichekesho kwa kuwa ndiyo fedha iliyolipa
kumpata kutoka Benfica ya Ureno.
Taarifa zinaeleza kuwa Kocha Tata
Martino wa Barcelona atakuwa tayari kuongeza dau la pauni milioni 31, ili
kumpata beki huyo.
Luiz sasa ni kati ya mabeki bora wa
kati katika Ligi Kuu England na Barcelona inafanya kila juhudi kumpata ili
kuziba pengo la Carles Puyol, nahodha wake wa zamani na beki imara zaidi wa
kati.









0 COMMENTS:
Post a Comment