August 15, 2013





Sakata la usajili wa Luis Suarez limeingia katika sura mpya baada ya Mruguay huyo kuzungumza na kusema hajui lolote kuhusiana na kubaki Livepool.

Suarez amekanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la El Observador la Uruguay ambalo lilimkariri kwamba amesema ameamua kusema anabaki.
Suarez amesema hakuzungumza na mwandishi yoyote kuhusiana na suala hilo, hivyo haikuwa sahihi.


Kauli yake hiyo ina maanisha kuwa bado ana mpango wa kuiacha Liverpool pamoja na kauli ya Kocha wake, Brendan Rodgers kumtaka aombe msamahe kwa wachezaji wote.


“Sikusema lolote kuhusiana na kubaki, labda alizungumza na mtu yoyote, kikubwa kwa sasa ni kwamba niko hapa na timu ya taifa na si zaidi,” alisema Suarez dakika chache baada ya mechi kati ya timu yake ya taifa ya Uruguay dhidi ya Japan kumalizika, yeye akiwa kati ya waliofunga.

Sakata la mshambuliaji huyo mbaguzi wa rangi limekuwa likiendelea kuchukua kura mpya na amekua akiwaeleza wazi kwamba anataka kuhamia Real Madrid ya Hispania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic