Chelsea imefikia hatua ya kutangaza dau
la pauni milioni 40 kumnasa mshambuliaji Wayne Rooney wa Man United.
Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho
ameendelea kusisitiza kutaka kumpata Rooney.
Taarifa zinaeleza kuwa Rooney naye
atakabidhi barua ya ombi lake kwa mara nyingine kutaka kuondoka.
Hali hiyo inamuweka kocha wa Man
United, David Moyes katika wakati mgumu.
Juhudi za Mourinho kuhusu Rooney
hazijapungua nguvu hata kidogo na amekuwa akitaka kumchukua mchezaji huyo.
Tokea Robin van Persie ajiunge na Man
United akitokea Arsenal, Rooney amekuwa katika wakati mgumu ikiwemo ni pamoja
na kuwa na uhusiano mbaya na kocha wa zamani Alex Ferguson.
0 COMMENTS:
Post a Comment