Timu ya 3Pillars Football Club ya
Nigeria sasa inaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki nchini baada ya kupata
idhini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF).
Awali tuliikatalia timu hiyo kucheza
mechi za kirafiki nchini kwa vile haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa
Shirikisho hilo limetoa idhini hiyo. Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na
wakala wa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) au mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Klabu hiyo kutoka Jimbo la Lagos
ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama cha mpira wa miguu cha jimbo hilo
ambacho nacho kilitakiwa kuomba idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.
Hivyo timu hiyo inaweza kucheza mechi,
kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) ambaye ni mwanachama wetu.
Tunapenda kukumbusha kuwa watu pekee
wanaotakiwa kuandaa mechi za kirafiki za kimataifa ni mawakala wa mechi
wanaotambuliwa na FIFA au wanachama wa TFF.








0 COMMENTS:
Post a Comment