Hatua ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya wakati.
Baadhi ya klabu zimefanya makosa madogo
madogo katika usajili ambapo zimepewa siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia
marekebisho kasoro hizo. Hivyo kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi
vyote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika Agosti 12
mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu
kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya pili ya usajili itaanza tena
Agosti 14 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika
Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania. Hivyo, dirisha la
uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya
usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.








0 COMMENTS:
Post a Comment