Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Joseph
Kimwaga, ambaye aliifungia timu yake bao la ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara dhidi ya Yanga, Jumamosi, amesema majeraha yalimnyima nafasi ya kucheza
Ulaya.
Kiungo huyo amesema alikuwa anatakiwa
kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Ureno.
Akizungumza na Championi Jumatano,
kiungo huyo alisema alipata dili la kwenda kufanya majaribio nchini Ureno,
lakini majeraha yakamnyima nafasi ya kucheza huko.
Kimwaga alisema klabu mbili zilijitokeza
zikimhitaji kwa ajili ya majaribio, hivyo hajakata tama, badala yake ataendelea
kufanya mazoezi kwa bidii ili kutimiza malengo yake ya kucheza soka la kulipwa.
“Hivi karibuni nilipata ofa ya kuitwa kwenye klabu
mbili za Ureno zikinihitaji kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa, lakini ilishindikana kutokana na majeraha yaliyokuwa yananisumbua.
“Bado sijakata tamaa ya kucheza soka la
kulipwa, ninaamini nitapata dili lingine la kwenda kucheza soka la kulipwa,
najua kuwa nina uwezo mkubwa wa kucheza soka, pia nimefurahi sana kumfunga
bingwa wa msimu uliopita wa ligi kuu,” alisema Kimwaga, 20.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga
kulala kwa mabao 3-2, Kimwaga aliifungia timu yake bao la tatu dakika za mwisho
kabisa za mchezo huo.








0 COMMENTS:
Post a Comment