| MANJI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA YANGA MSIMU ULIOPITA, LEO AMEKUTANA NA KIKOSI HICHO TENA KWENYE HOTELI YA SERENA JIJINI DAR |
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
amekutana na wachezaji wa kikosi cha Yanga usiku huu.
Manji amekutana na wachezaji hao
pamoja na benchi la ufundi ambalo limeongozwa na Kocha Mkuu, Ernie Brandts.
Mkutano huo wa kimyakimya ambao
waandishi wa habari hawakutakiwa kuhudhuria umefanyika kwenye hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, Manji
amezungumza mambo mbalimbali na wachezaji hao ikiwa ni pamoja na suala la
kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC.
Yanga iliyocheza vizuri katika mechi
hiyo, ilipoteza kwa kuchapwa mabao 3-2.
“Lengo la mwenyekiti lilikuwa ni
kuhakikisha tunaangalia wapi tumejikwaa na baada ya hapo tunaendelea mbele.
“Kikubwa amesisitiza kuangalia zaidi
ushirikiano na kwamba sisi ni mabingwa hivyo lazima tupambane bila ya kujali
timu zinatupania kupita kiasi,” alisema mtoa habari.
Wachezaji takribani wote wa Yanga
walihudhuria mkutano huo na baadaye walipata chakula cha usiku pamoja.







0 COMMENTS:
Post a Comment