September 23, 2013





Mario Balotelli amekosa penalti ya kwanza katika maisha yake ya soka huku kikosi chake cha AC Milan kikipoteza mechi ya Serie A kwa kuchapwa 2-1 na wageni wao Napoli.


Kipa wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina ambaye sasa anakipiga Napoli ameingia kwenye rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kuokoa mkwaju wa penalti ya Balotelli baada ya Muitalioano huyo kuwa amefunga mara 21 bila ya kukosa.




Baada ya mechi hiyo, Super Mario alikuwa na kutaka vurugu hivyo kuwalazimu wenzake kufanya kazi ya ziada kumzuia.

Moja ya mabao ya Napoli yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Gonzalo Higuain ambaye sasa amekuwa lulu ya Napoli.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic