Javier Harnandes
amefunga bao pekee katika mechi ya Kombe la Capital One raundi ya tatu kati ya Liverpool dhidi ya Man
United.
Man United waliokuwa
nyumbani OT walipata ushindi huo wa bao 1-0 baada ya kona iliyochongwa na Wayne
Rooney kumpita Steven Gerrard na kutua mguuni mwa Chicharito.
Ukichana na bao hilo,
mchezo wa timu zote ulilingana na mashambulizi yalikuwa ya zamu.
Luis Suarez aliyekuwa
amerejea Liverpool kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa ya
FA, alionyesha yuko fiti lakini hakuweza kuisaidia Liverpool kusawazisha.
Mara moja mpira wa
adhabu wa Mruguay huyo ulipalaza mtambaa wa panya na wakati mwingine kipa David
De Gea akaokoa mpira wa kichwa wa karibu kabisa wa Victor Moses.
Kwa upande wa
Arsenal, wao walitotoka sare ya bao 1-1 dhidi wa Wes Brom Albioni katika kali
ya kusisimua.
Vijana hao wa Wenger
walikuwa ugenini na bao lao lilifungwa na Thomas Eisfeld na wenyeji
wakasawazisha kupitia Thomas Seido.
Kutokana na matokeo hayo, waliongezewa muda wa dakika 30 ili kupata mshindi, hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa bado 1-1.
MATOKEO MENGINE CAPITAL
ONE
Birmingham 3 Swansea 1
Newcastle 2 Leeds 0
Tranmere 0 Stoke 1








0 COMMENTS:
Post a Comment