Kiungo nyota wa
Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’ amelazimika kuondoka katika kikosi hicho kwa muda.
Uongozi wa Yanga
umempa Chuji ruhusa ya siku mbili kwenda kumzika shangazi yake mjini Mpwapwa
mkoani Dodoma.
“Kweli Chuji amefiwa
na shangazi yake na anakwenda kushiriki mazishi.
“Amepewa ruhusa na
baada ya hapo atarejea na kuungana na wenzake,” alisema Meneja wa Yanga, Hafidh
Saleh.
Chuji ni kati ya viungo
wakongwe wa Yanga na amekuwa tegemeo katika kuituliza na uchezeshaji wa timu.








0 COMMENTS:
Post a Comment