| CHUJI KATIKA MAZOEZI YA LEO |
Baada ya ruhusa ya siku
mbili, kiungo Athumani Idd ‘Chuji’ amerejea katika mazoezini ya kikosi cha
Yanga.
Chuji alifanya mazoezi na
wenzake leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar.
Mazoezi hayo yalikuwa ya
misho kabla ya Yanga kuivaa Ruvu Shooting, kesho jijini Dar.
Kiungo huyo alipewa
ruhusa ya siku mbili kwenda mjini Mpwapwa mkoani Dodoma kumzika shangazi yake.
Kuhusiana na kucheza,
inaonekana kesho Kocha Ernie Brandts atampanga kinda Frank Domayo kwa kuwa
kiungo huyo mkongwe hakuwa na wenzake kwa siku mbili.







0 COMMENTS:
Post a Comment