Hatimaye mshambuliaji Mrisho Ngassa
amemalizana na Simba baada ya kuzikabidhi Sh milioni 45 kwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), leo.
Ngassa amesema amewasilisha fedha hizo
kwa TFF na Simba watalipwa na shirikisho hilo.
Ngassa aliongozana na mjumbe wa
sekretalieti ya Yanga, Patrick Naggi na kukabidhi fedha hizo katika kitengo cha
fedha cha Yanga.
“Kweli nimemalizana nao, sasa naelekeza
nguvu zangu katika kuisaidia Yanga,” alisema Ngassa.
Ngassa alitakiwa kulipa Sh milioni 45
baada ya kuchukua Sh milioni 30 za Simba. Sh milioni 15 imekuwa ni adhabu.








0 COMMENTS:
Post a Comment