DHAIRA MAZOEZINI SIMBA |
Kipa namba
moja wa Simba, Abel Dhaira amesema bado anasikia maumivu katika kiwiko cha
mkono wa kushoto na kudai kuwa amepanga kwenda nchini Iceland barani Ulaya
kupata matibabu zaidi kwa daktari anayeamini atamtibu.
Dhaira
raia wa Uganda amesema licha ya kupata matibabu mara mbili akiwa hapa nchini na
hata yale aliyoyapata wiki moja iliyopita Uganda, bado hayajamaliza tatizo hilo.
Dhaira amesema
amepanga kutua nchini Iceland mwezi ujao endapo atapata ruhusa kutoka kwa
uongozi wa Simba, ambapo huko kuna daktari mzuri ambaye tayari ameshazungumza
naye tayari kwa kumtibu vizuri tatizo hilo.
“Bado
nasikia maumivu katika kiwiko, nimepata matibabu kwa nyakati tofauti hapa
Tanzania na hata hivi karibuni nilivyorudi nyumbani (Uganda), lakini bado
hayajasaidia kama nilivyokuwa nategemea,” alisema Dhaira ambaye amejiunga na
Simba msimu huu akitokea IBV ya Iceland.
Mpango
huo wa Dhaira, unakuja kufuatia kuumia mwezi uliopita wakati akiwa katika
mazoezi ya timu hiyo, katika kambi yao iliyopo kwenye Fukwe za Bamba, nje
kidogo ya Jiji la Dar, eneo la Kigamboni.
0 COMMENTS:
Post a Comment