Kocha Mkuu wa Mgambo Shooting, Mohamed
Kampira amesema kuwa bado hajashawishiwa na kiungo mchezeshaji mpya wa timu
hiyo, Mohamed Samatta, ambaye ni kaka wa mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo,
Mbwana Samatta.
Kampira amesifu kiwango cha kiungo huyo huku akimtaka kuendelea kumshawishi kwa kuonyesha kiwango kizuri ndani ya uwanja.
“Akiwa anaichezea African Lyon alikuwa
yupo kwenye kikosi cha kwanza, lakini hapa Mgambo amekutana na wachezaji
waliomshinda na kusababisha kumuweka benchi.
“Amekutana na ushindani mkubwa,
anahitaji anishawishi ili nimuweke kwenye kikosi changu cha kwanza
kinachoshiriki ligi kuu,” alisema Kampira.
0 COMMENTS:
Post a Comment