Mashabiki wa Besiktas wamevamia uwanja na kufanya vurugu kubwa zilizosababisha mechi dhidi ya wapinzani wao wakubwa Galatasaray kuvunjika katika dakika ya mwisho.
Wakati mechi hiyo inavunjika dakika ya tatu ya nyongeza huku Galatasaray ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1, yote yakiwa yametupiwa kimiani na mshambuliaji Didier Drogba.
Mashabiki wa Besiktas walianzisha vurugu baada ya kiungo na nahodha wa Galatasaray, Felipe Melo baada ya kumrukia kwa miguu miwili mchezaji wa Besiktas na kulambwa red card.
Pamoja na kadi hiyo nyekundu, mashabiki hao hawakuridhika, waliamua kuingia uwanjani na kulazimisha wachezaji wote na waamuziki kukimbilia vyumbani.
Vurugu hizo zilikuwa kubwa baada ya mashabiki hao kuwazidi nguvu walinzi uwanjani hapo.
Kabla, Besiktas walitangulia mbele kwa bao la Hugo Almeida katika dakika ya 18, lakini Drogba akasawazisha na kuongeza la ushindi.














0 COMMENTS:
Post a Comment