Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limetangaza ratiba
ya mwisho ya michuano ya timu za Afrika kuwania kucheza Kombe la Dunia mwakani
nchini Brazil.
Ivory Coast watakuwa na kibarua kigumu katika
mechi hizo mbili za mwisho watakapocheza dhidi ya Senegal.
Nigeria imepangiwa Ethiopia wkati Ghana
itapambana na Misri, vigogo wanaoonekana kupotea mwelekeo lakini si vema
kuwadharau.
Kwa mujibu wa Caf, mechi hizo zitachezwa
nyumbani na ugenini na zile za kwanza nikipgwa kati ya Oktoba 11-13 na
kurudiana kati ya Novemba 15-19.
Iwapo timu zitatoka sare katika mechi zote
mbili, basi zitaongezewa dakika 30 na ikiwa bado hakuna mshindi, mikwaju ya penalty
itafuatia.
Mechi zote tano ambazo zitatoa timu za Afrika
zitakazoshiriki Kombe la Dunia Brazil, hizi hapa;
Ivory Coast Vs Senegal
Tunisia Vs Cameroon
Ethiopia Vs Nigeria
Ghana Vs Egypt
Burkina Faso Vs Algeria
0 COMMENTS:
Post a Comment