September 16, 2013



 
CHEKA AKIWA NA SALEH ALLY
Bingwa wa Dunia Mkanda wa WBF uzito wa super-middle, Francis Cheka, amezawadiwa viwanja viwili na serikali ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni zawadi na pongezi baada ya kufanikiwa kutwaa mkanda huo mkubwa duniani, hivi karibuni.


Cheka alifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa dunia baada ya kumchakaza kwa pointi aliyekuwa akiushikilia ubingwa huo, Mmarekani Phil Williams katika pambano lililopigwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar, Agosti 30, mwaka huu.

Cheka alipewa viwanja hivyo kwa nyakati tofauti mkoani Morogoro ambapo kimoja kipo Segera, Mvomero na kingine kipo Morogoro mjini.
Joel Bendera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, alimkabidhi Cheka kiwanja kilichopo Morogoro mjini chenye thamani ya shilingi milioni sita kwa niaba ya manispaa ya mkoa huo huku wananchi wa mkoani humo wakiahidi kumjengea nyumba kwenye kiwanja hicho.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Cheka alisema amefurahia zawadi hiyo na amejisikia faraja kuona serikali inatambua umuhimu wake.

 “Nashukuru sana kwa kweli kwa viwanja hivi, kimoja kipo Segera, Mvomero, bado sijakiona ila hiki kingine cha mjini tayari nimeshakabidhiwa hati na kila kitu,” alisema Cheka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic