Kipindi cha pili kimeanza na Ramadhani Singano 'Messi' anaipatia Simba bao la pili katika dakika ya 50.
&&&&&&&&&
&&&&&&&&&
Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe
amefunga bao moja na kuifanya Simba imalize kipindi cha kwanza ikiongoza kwa
bao 1-0.
Bao hilo la Tambwe ni la mkwaju wa penalty
baada ya beki mmoja wa JKT kuunawa mpira wakati akijaribu kuokoa.
Sasa Tambwe amefikisha mabao saba akiendelea kuongoza katika upachikaji mabao.
Kipindi cha kwanza kimekuwa cha
mashambulizi ya zamu kila upande, ingawa Simba ndiyo waliopoteza nafasi tatu za
kufunga huku JKT wakipata moja.
Mpira haukuwa na mvuto sana katika
kipindi hicho kutokana na wachzaji wa timu hizo kupoteza pasi nyingi sana kila
mara.
Sasa timu zimo ndani ya vyumba zikipata
mawaidha ya makocha wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment