Kocha Tata Martino ameweka
rekodi mpya ya kushinda mechi saba mfululizo za La Liga.
Martino maarufu kama Tata
ameshinda mechi saba mfululizo baada ya jana kikosi chake kuichapa AlmerÃa kwa
mabao 2-0.
Mabao hayo yaliyofungwa na
Messi na Adriano yameifanya Barca kuendelea kujichimbia kileleni.
Kabla, mechi za kwanza
zilikuwa ngumu kwa makocha wengi na ngumu kushinda mfululzio.
Tata amejiunga na timu hiyo
akitokea nchini Argentina na amechukua nafasi ya Tito Vilanova aliyelazimika
kupumzika kutokana na maradhi ya kansa.
Katika mechi hiyo, pamoja na
kufunga bao la kwanza, dakika chache baadaye Messi alitolewa baada ya kuumia.
Kuumia kwake kumezuua hofu
huenda akazikosa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment